Saturday, December 5, 2015

Anonymous

Anachofanya Waziri Mkuu, Sio Sawa, Sio Haki, Sio Good Governance...Ni Udhalilishaji na Kuaibishana! Maoni ya Mdau Mwenzenu Nawe Changia Hoja Hii Tafadhali....

Kwanza naomba kukiri, kuwa ninaunga mkono kwa asilimia 100% juhudi za serikali awamu ya 5 kupambana na rushwa, ufisadi, uzembe na ukwepaji kodi, ili mtindo unaotumiwa na Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kassim Majaliwa, sio!.

Baada ya kukisikia kisanga cha TRA kilichomng'oa Kamishna Mkuu na maofisa kadhaa kufuatia sakata la makontena, leo amerudi tena bandarini na nimekishuhudia kitu anachokifanya, japo anashangiliwa na umati wa watu, lakini anachokifanya ni kuviziana, kutishana, kudhalilishana na kunakwenda kinyume cha utawala bora, yaani good governance!.

Waziri Mkuu anafanya ziara za kushtukiza mahali, huku akiwa na karatasi lenye tuhuma specific, lakini amelificha!, anakwenda kumuuliza mhusika wa pale kuhusu utendaji wa mfumo fulani, anaelezwa kuwa mfumo uko perfect, kisha analiibua hilo karatasi lenye tuhuma na kuanza kumsomea mhusika mbele ya kadamnasi ya watu, abcd!, mhusika anashindwa kujibu, atasimamishwa kazi, na kama yuko juu ya mamlaka yake, atamchongea kwa Rais!.

Hata TRA siku hiyo alikwenda na nondo za makontena, alipomuuliza Bade, akamjibu details ziko kwa maofisa wangu, ndipo akaibua nondo lake na kumsomea kwenye kadamnasi ili aonekane mjinga!, huku ni kuaibishana, kudhalilishana na kinyume cha good governance!.

Baada ya kutoka bandaini, akaenda TRL na kumuuliza mkurugenzi mkuu, mlikopa bilioni 3 TIB za kufanyia nini?!, kwa nini hamkufanya kile mlichokopea?, akaambiwa tumelipia mishahara, nani aliwapa idhini ya kukopa?!, Mkurugenzi hana jibu na naamini kesho atatangazwa hana kazi!.

Top management angekaa nao ofisini na kuulizana kistaarabu ndio good governance!. Mimi hata home, wife alikuwa na tabia ya kuwafokea ma tx home, mbele ya watoto, nikamkataza!, nikamsisitiza if things are not right, muite pembeni ndipo umseme, sio kumdhalilisha mbele ya watoto!.

Anachofanya Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kasim Majaliwa ni kuviziana, kudhalilishana na kuabishana bila sababu za msingi!, hili la kuitana na kuanza kuhojiana mbele ya waandishi ili watu wamuone alivyo mkali, ni tabia za ma populist leaders!, Leo nimemuona Magufuli akiongea na wafanyabiashara yuko very humble even cracking some jokes!.

Kama kuna watu wako karibu na Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kasim Majaliwa, wamwambie anavyofanya sio vizuri, Sio Sawa, Sio Haki, Sio Good Governance!, Ni Udhalilishaji na Kuaibishana tuu!. Akumbushwe kuna kitu kinatwa 'karma' kisije kumshukia!.
Au wewe unaonaje?! Toa maoni yako ni sawa au sio sawa!.
By Pasco-Jamii Forums

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

1 comments:

Write comments
Unknown
AUTHOR
December 5, 2015 at 2:48 PM delete

Kwanza naona wewe hauna akili hata kidogo, nadhani wewe ndiyo waleee wenye makontena zaidi ya 2000, una nyumba 73, unaweka pesa kwenye ndoo. mm hapa hata buku mfukoni sina, sijui kiwanja cha kujenga nyumba nitakipata wapi kwa gharama gani? wao mbona walikuwa wanaiba mchana kweupe? kwa nn walikuwa hawana huruma? unajua akina mama wajawazito wangangapi wamekufa kwa kukosa dawa? watoto wangapi wamekufa? wagonjwa wangapi wamekufa? hivi unatumia akiri wewe ulitoa maoni hayo? nakuomba kaa kimya? ningelikuwa mm ni waziri mkuu naamua wanyongwe papohapo? na hapo kawapoozea? namshauri waziri mkuu wangu ongeza spidi, kaza buti, endelea moto huo, HAPA KAZI TU.

Reply
avatar

Note: Only a member of this blog may post a comment.