MSANII wa filamu Bongo, Haji
Adamu ‘Baba Haji’ amesema kampeni za siasa zilizokuwa zikifanyika
kuelekea uchaguzi mkuu uliopita, zimemkosesha kupata mtoto kwa vile
alikuwa mbali na mkewe aliyebaki Dar.
Akizungumza na gazeti hili, alisema
alipata mtoto mmoja wa kiume katika uhusiano wake kabla hajamuoa
mwanamke huyo, lakini akakosa amani kwa sababu ya hamu yake ya kupata
mtoto wa kike.
“Natamani hata kesho mke wangu anizalie
mtoto wa kike yaani namsaka kwa udi na uvumba, huenda ningekuwa
nimeshampata lakini mambo ya uchaguzi yalisababisha zoezi langu lisiende
na wakati, sababu muda mwingi nilikuwa bize kwenye mambo ya kampeni
huku bibie akibaki Dar wakati mimi nikizunguka mikoani, hivyo sasa hivi
nafanya jitihada za hali ya juu,” alisema.

Note: Only a member of this blog may post a comment.