Monday, November 16, 2015

Anonymous

Vijana Wasusa Kupiga Kura Jimbo la Lulindi Kisa LOWASSA!

Kushindwa kwa mgombea wa urais wa Chadema kupitia Ukawa, Edward Lowassa kumesababisha vijana wengi katika Jimbo la Lulindi mkoani Mtwara kususia uchaguzi mdogo wa mbunge jana.
 
Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya vijana wa jimbo hilo, Jafari Hamisi, Nurudini Majaliwa na Saidi Mohamed walisema sababu kubwa ya kususia kuchagua mbunge ni kutoridhishwa na mfumo wa siasa ambao walidai hauzingatii demokrasia ya vyama vingi, bali umeegemea chama kimoja pekee.
 
Mkazi wa Kata ya Lulindi, Anasa Hussein alisema watu wengi wamekatishwa tamaa kutokana na kuahirishwa kwa uchaguzi huo Oktoba 25.
“Mimi kwa upande wangu sikujua leo kama unafanyika uchaguzi wa mbunge, nilikuwa najiandaa kwenda shambani, nikasikia watu wanasema leo ni siku ya uchaguzi, " alisema Anasa.
 
Msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo hilo, Beatrice Dominic amekiri kuwapo mwitikio mdogo wa wapiga kura licha ya kufanya uhamasishaji mkubwa.
 
Msimamizi wa Kituo cha Zahanati ya Chiungutwa, Romanusi Charles alisema mwamko wa kupiga kura ulikuwa mkubwa kwa vijana katika uchaguzi wa Oktoba 25 kwani wengi walijitokeza tofauti na jana.
 
Mgombea ubunge wa NLD, Modester Makaidi alisema katika vituo ambavyo alitembelea, vijana walishindwa kujitokeza kutumia haki yao ya msingi ya kupiga kura.
Mgombea wa CCM, Jerome Bwanausi jana asubuhi aliendelea kusisitiza wananchi kujitokeza kupiga kura katika vituo vyao.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.