Monday, November 16, 2015

Anonymous

Rais Dkt. John MAGUFULI Amteua Naibu Mwanasheria Mkuu Dkt. Tulia Ackson Mwansasu Kuwa Mbunge

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli, leo asubuhi ametengua uteuzi wa Naibu Mwanasheria Mkuu Dr Tulia Ackson, Mwansasu na kumteua kuwa Mbunge.
Msemaji wa Serikali ya Tanzania, Assah Mwambene, amethibitisha kutenguliwa na kuteuliwa kwa Dk. Tulia.

Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Thomas Kashilila, amekiri kupokea taarifa ya uteuzi wa Dk. Tulia mapema leo asubuhi.

Awali kabla ya uteuzi huo, Dr Tulia alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ambapo pia hapo jana Novemba 15, 2015 alikuwa ameteuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea nafasi ya Spika wa Bunge.

Soma tamko la bunge kuhusu uteuzi huo hapa

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.