Saturday, November 7, 2015

Anonymous

VIDEO+PICHAZ: Mabingwa CHELSEA Wazidi Kutia AIBU Uingereza...Shuhudia Ilivyochapwa na Stoke City Leo November 7

lkiwa huu unatajwa kuwa mwaka mbaya kwa kocha wa Chelsea Jose Mourinho kutokana na mwenendo mbovu wa kikosi chake msimu huu, walilazimika kusafiri kuifuata klabu ya Stoke City kucheza mchezo wake wa 12 wa Ligi Kuu Uingereza msimu huu, klabu hiyo ambayo ni Bingwa mtetezi wa Ligi Kuu Uingereza huenda wakashindwa kutetea ubingwa wao.
2672
Chelsea ambayo kwa sasa haina matokeo mazuri uwanjani tofauti na miaka ya nyuma, iliingia uwanjani bila ya kuwa na kocha wao huyo mreno Jose Mourinho kutokana na kutumikia adhabu yake ya kufungiwa mchezo mmoja kwa kosa alilolifanya katika mchezo kati ya Chelsea dhidi ya West Ham United kuwatolea lugha chafu waamuzi wa mchezo huo wakati wa mapumziko.
274977C100000578-0-Chelsea_winger_Hazard_left_holds_off_Stoke_City_s_Geoff_Cameron_-a-31_1428166921861
Chelsea waliokuwa nafasi ya 15 katika msimamo wa Ligi Kuu Uingereza kwa jumla ya mechi 11, wamepoteza mchezo huo kwa mara nyingine tena na kushuka hadi nafasi ya 16, Stoke City wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0, goli ambalo lilifungwa na Marko Arnautovic  dakika ya 54 na kudumu kwa dakika zote 90.
Video ya magoli ya Stoke City Vs Chelsea hii hapa

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.