UTATA: TB Joshua Azua SINTOFAHAMU Kubwa Nchini, Ni Baada ya Kuyeyuka Ghafla!
Muhubiri wa kimataifa nabii maarufu duniani Temipote Balogun maarufu kama TB Joshua ameacha maswali baada ya kushindwa kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa rais mpya wa awamu ya tano Dk.John Magufuli.
TB Joshua aliwasili nchini November 03 kwa ndege binafsi na kupokewa na Dk.MAGUFULI pamoja na Mbunge mteule Mwigulu Nchemba katika uwanja wa kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere,Dar es salaam.
Baada ya kuwasili alifanya mazungumzo ya faragha na Dk.MAGUFULI
pamoja na rais mstaafu Jakaya Kikwete kisha kufanya mazungumzo zaidi ya
saa tatu na Edward Lowassa.
Ujio wa nabii huyo ulionekana kama amekuja kwa ajili ya kuapishwa kwa
Dk.Magufuli lakini huku baadhi ya wananchi wakifurahishwa na ujio wake
na kuamini ni fursa pekee ya kukutana naye na kufanya maombi akiwa hapa
nchini.
Baadhi ya watu walisema waliamua kwenda uwanja wa Uhuru kwa ajili ya
kumuona nabii huyo lakini haikuwa hivyo na hawakufahamu kwa nini
hakuhudhuria sherehe hizo.
USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK
TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)
Note: Only a member of this blog may post a comment.