Imelda mtema
Lady Gaga wa Bongo, Faiza Ally ambaye
amezaa na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi amefungukia ushindi wa
mzazi mwenzake huyo na kudai kuwa haumsaidii chochote.
Akizungumza juzi na Ijumaa, Faiza
alisema alivyosikia ushindi wa Sugu wala hakufurahi kwani alimchukulia
kama mtu mwingine tu aliyeshinda.
“Mimi kwa kweli ushindi wa Sugu naona
kama wa mtu mwingine, haunihusu wala kunisaidia chochote mimi na
mwanangu. Yeye ana maisha yake na sisi tuna maisha yetu hivyo nikisema
eti nimefurahi yeye kushinda nitakuwa nawadanganya,” alisema Faiza.

Note: Only a member of this blog may post a comment.