Tuesday, November 3, 2015

Anonymous

TAARIFA Kuhusu Maandamano ya CHADEMA Kumpinga MAGUFULI Jijini MWANZA

JESHI la Polisi mkoani Mwanza, limepiga maarufuku maandamano ya amani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ya kupinga matokeo yaliyompa ushindi, Rais mteule wa awamu ya tano, John Magufuli.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa mwanza, Kamishna Msaidizi, Charles Mkumbo, wakati akizungumza na waandishi wa habari, ambako alisema ni marufuku kwa mtu yeyote yule kuandama LEO.

Alisema licha ya chama hicho kufikisha barua ya kuomba kibali cha kufanya maandamo ya kupinga matokeo ya Magufuli na kwamba Polisi hawatasita kuwachukulia hatua za kisheria wale wote watakao fanya maandamano.

Mkumbo alisema kuwa endapo mtu ama kikundi chochote kile kitabainika kufanya maandamano, watakuwa wamevunja sheria za nchi, hivyo Polisi haitaka kuwa nyuma kuwachukulia hatua za kisheria.
Hata hivyo Mkumbo alidai kwamba Rais mteule, John Magufuli amechaguliwa na wananchi walio wengi na kutangazwa na Tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC), iweje watu wachache wapinge matokeo hayo.

“Wao wanadai eti… mgombea wao ndiye kashinda (Edward Lowassa), kwamba hawakubaliani na matokeo hayo, sasa maandamano yoyote yale ni maarufuku kufanyika hapa Mwanza,” alisema Mkumbo.

Hata hivyo, Katibu wa Chadema, Wilaya ya Nyamagana, Rehema Mkoha, amesisitiza kufanyika kwa maandamano hayo leo na wamejipanga kupinga matokeo hayo.
“Sio kila kitu mpaka uruhusiwe na ukipigwa maarufuku ndo uache kufanya maandamano, hapa ninapoongea na wewe tupo kwenye kikao cha kutoa maamzi ya kufanya kesho (leo) maandamano,” alisema Rehema.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.