Wakati michuano ya Kombe la Shirikisho inaanza rasmi leo ikishirikisha timu 64 za Ligi Kuu, Daraja la Kwanza na la Pili, uongozi wa Simba unaonekana kutoipa kipaumbele.
Mabingwa hao mara 18 wa Bara wamesema akili yao kwa sasa iko katika kusaka ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara na si mashindano hayo ya Kombe la Shirikisho ambayo bingwa wake ataiwakilisha Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika 2017.
Rais wa Simba, Evans Aveva, aliiambia Nipashe jijini Dar es Salaam jana kuwa wako katika mkakati wa kuhakikisha wanalitumia dirisha dogo la usajili kuboresha kikosi chao kwa kusajili beki wa kati na mshambuliaji wenye viwango vya kimataifa.
Dirisha dogo la usajili litafunguliwa rasmi Novemba 15 na kufungwa Desemba 15 mwaka huu.
Aveva alisema usajili huo ni sehemu ya utekelezaji wa mapendezo ya kocha wao Muingereza Dylan Kerr kabla ya kuanza tena kwa ligi ya Bara iliyosimama kupisha maandalizi ya mechi za Taifa Stars dhidi ya Algeria.
"Lengo letu kuu ni kutwaa ubingwa wa Tanzania Bara, na hilo Kombe la Shirikisho tunaweza pia, lakini akili na mawazo ya Simba sasa ni kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu," alisema Aveva.
Simba na timu nyingine za Ligi Kuu zitaanza kampeni ya kuwania ubingwa wa Kombe la Shirikisho katika raundi ya tatu. Mashindano hayo yaliyorejeshwa mwaka huu, yanaendeshwa kwa mtindo wa mtoano.
Katika hatua nyingine, Rais huyo na Mwenyekiti wa zamani wa Kundi la Friends of Simba, aliweka wazi kuwa wanawafuatilia kwa karibu washambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Laudit Mavugo na Kevin Ndayisenga.
Simba ilitaka kumsajili Mavugo kabla ya kuanza kwa msimu huu wa Ligi Kuu, lakini usajili wake ulishindikana kutokana na dau kubwa ambalo klabu yake ilihitaji.
"Kuhusu beki wa kati, tumeanza mchakato kuhakikisha tunapata mwenye kiwango cha juu na atakayekuwa msaada kwa timu yetu," alisema zaidi Aveva.
Simba inayokamata nafasi ya nne katika msimamo wa ligi ya Bara, imekuwa inawategemea zaidi mabeki wa kati Hassan Isihaka na Juuko Murshid katika safu ya ulinzi na wakati mwingine imekuwa ikimtumia kiungo Mzimbabwe Justice Majabvi kwenye nafasi hiyo.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

Note: Only a member of this blog may post a comment.