Monday, April 13, 2015

Anonymous

PICHAZ na VIDEO: Tazama ndoa ya mama yake BEYONCE mbayo ni gumzo duniani kwa sasa!


tina 
Niliwahi kukusogezea hapahapa story kuhusu talaka ya mama wa staa wa mitindo duniani Kim Kardashian ambaye aliamua kuchana na mumewe Bruce Jenner, leo mama wa staa mwingine wa muziki kajaa kwenye HEADLINES tena.. nae anaolewa. 

Tina Knowles mama wa Beyonce, kibongobongo wangeongeza neno hapo, mama mkwe wa Jay Z nae kaona aachane na ubachela wa uzeeni, duh.. kafunga ndoa na actor Richard Lawson

Wale wale mabingwa wa udaku wa mastaa duniani mapaparazzi wa TMZ.. ambao ndio waliokuwa wa kwanza pia kutoa VIDEO ya Jay Z akipigwa mateke na Solange kwenye lift, ndio waliotoa PICHAZ na video za event hiyo ya nguvu iliyofanyika katika fukwe za California.
tina 2 
Unaambiwa wageni wote walikuwa wamevaa nguo nyeupe; ilikuwa All White Ceremony ilikuwa ni ndoa ya pili kwa mama huyo mwenye miaka 61.

Watu wa karibu walihudhuria party hiyo, mapaparazzi wanasema boti ina uwezo kubeba watu 300 tu, kwa hiyo idadi ya wageni haikuzidi namba hiyo.

Jay Z, Beyonce na mtoto wao Blue Ivy. nao walikuwa sehemu ya party hiyo.

tina

Tina na mzee Mathew Knowles walipeana talaka mwaka 2009, hapo ilikuwa miaka 30 tangu wafunge ndoa yao.. halafu uhusiano wa Richard na Tina ukaanza 2013.

jay

tina3

Richard Lawson na Tina Knowles
-via millardayo

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.