Kati ya maagizo Rais aliyoacha ni pamoja na mashine za CT Scan pamoja na MRI kuhakikisha zinatengenezwa ndani ya wiki mbili.
Mkuu wa kitengo cha mawasiliano ya umma Aminiel Eligaisha amesema baada ya kukutana na kamati tendaji ya hospitali hiyo leo na Kaimu Mkurugenzi aliyeteuliwa Prof.Lawrence Mseru ametoa maelezo na kuhakikisha watafanyia kazi maagizo yaliyotolewa na Rais ndani ya muda waliopewa.
Wagonjwa wanaotumia mashine za MRI kwa siku ni wagonjwa 10 hadi 15 na kila mgonjwa hutumia zaidi ya dakika 40 kutumiwa na kipimo cha CT Scan wagonjwa wenye uhitaji ni kati ya 20 hadi 25..“Wagonjwa wamekuwa wakipata taabu sana baada ya mashine hizi kuharibika na imewabidi kwenda hospitali binafsi ili kuweza kupata vipimo ambavyo huku ni gharama zaidi ya hapa” Eligaisha.
Amesema kwa sasa wanafanya juu chini kuhakikisha agizo hilo linatekelezwa kwa wakati ili wananchi waweze kupata huduma hiyo.
Pia amesema Serikali ndiyo ilisaini mkataba wa kutengeneza mashine hizo na ndio sababu wameweza kulipa fedha kwa ajili ya matengenezo hayo.

Note: Only a member of this blog may post a comment.