Mwambene (kushoto) akisikiliza maswali yaliyokuwa yakiulizwa na wanahabari (hawapo pichani).
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo), Assah Mwambene, alipokuwa akizungumza na wanahabari kuwa kwa mujibu wa tamko la Rais Dk. John Magufuli, siku hiyo itumike kufanya usafi hivyo itakuwa siyo siku ya kwenda kazini.
Amesema anatambua kuwa kila mwananchi au mtumishi wa umma anayo sehemu anayoishi katika kijiji, kata, wilaya na hata mkoa, hivyo atapangiwa maelekezo ya kusafisha eneo husika kupitia viongozi wa serikali za mtaa husika.
Amesema kuwa viongozi wa serikali za mitaa wanaendelea kupewa maelekezo ya kuainisha maeneo ambayo yamekithiri kwa uchafu ili siku hiyo kuhakikisha yanasafishwa.
Amebainisha taarifa zinazotolewa kwenye mitandao ya kijamii ya kuwa wafanyakazi wa utumishi wa umma wataenda kazini siku hiyo si za kweli bali ni kutaka kupotosha umma.
(NA DENIS MTIMA/GPL)

Note: Only a member of this blog may post a comment.