Good Morning mtu wangu, Uchambuzi wa magazeti redioni @CloudsFM
umekupita? Kazi yangu siku zote ni kuhakikisha zile zote kubwa za siku
zinakufikia, hizi ni baadhi ya stori zilizoguswa kwenye Uchambuzi
redioni.
Rais John Magufuli atua Bandarini, TPA yapunguza watendaji 30, pepo la ukwepaji kodi lafika mwisho, Mashine za kipimo cha MRI zaharibika tena Muhimbili, Edward Lowassa Seif awatesa CCM, wachimbaji waokolewa baada ya kufukiwa ardhini kwa siku 41 na nyumba 45 za bomolewa Dar es salaam, Kurasini.
Wiki moja baaada ya kutengenezwa kwa mashine za MRI katika Hospitali ya Muhimbili, mashine hizo zaharibika tena katika hospitali hiyo jana baada ya kuwahudumia wagonjwa 21… BAVICHA imetoa siku tatu kwa jeshi la polisi kuwafikisha Mahakamani wale wote waliohusika kwenye mauaji ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Geita.
Baada ya kufanya matembezi kwenye hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kukagua mashine za MRI, Rais John Magufuli amefanya ziari nyingine Bandarini na kukagua mashine za kupima mafuta na kisha kuzitaka zianze kufanya kazi, awali zilizokuwepo zilikatazwa na wakala wa vipimo WMA kutumika kwa madai ya kuwa zinawapunja wateja.
Wakati Bunge la 11 likitegemea kuanza
vikao vyake leo, kuna taarifa ya kuwepo kwa kile kinachodaiwa kuwa
mvutano wa chini chini baina ya Waubunge wa CCM na Rais Dk. John Magufuli kuhusu nani anaestahili kupitishwa kuwa mgombea wa nafasi ya Naibu Spika huku Job Ndugai apitishwa bila kupingwa… Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA wamemteua, Goodluck Ole Medeye kutoka CHADEMA kusimama katika nafasi ya uspika.
Note: Only a member of this blog may post a comment.