Mchungaji huyo akiwa chini ya ulinzi pamoja na wenzake.
Makongoro Oging’ na Haruni Sanchawa
UHALIFU! Mchungaji kutoka Nigeria, Chid
Okechukwi aliyekamatwa na kikosi kazi (task force) cha kudhibiti na
kupambana na madawa ya kulevya nchini akiwa na kilo 81 za madawa ya
kulevya aina ya cocaine amehukumiwa kwenda jela miaka 30 na faini ya
shilingi bilioni tisa akitoka mwaka 2045.
Taarifa kutoka vyanzo vyetu makini na kuthibitishwa na Mkurugenzi wa Mashtaka Tanzania (DPP), Diswalo Mganga zinasema mchungaji huyo alihukumiwa Ijumaa ya wiki iliyopita na Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, Mheshimiwa Huruma
“Nimeshuhudia kesi nyingi za zamani zinazohusiana na madawa ya kulevya zimetolewa hukumu na wahusika wamefungwa kwa waliopatikana na hatia. Kasi hii ni nzuri, napongeza mahakama,” alisema Nzowa.
Kesi za kukutwa na madawa ya kulevya kwa sasa zimepamba moto ambapo hivi karibuni, Fred William Chonde alihukumiwa kwenda jela miaka 20 na faini ya shilingi bilioni 15 akitoka mwaka 2035.
Note: Only a member of this blog may post a comment.