Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza kesho mchana inatarajiwa kutoa hukumu ya
kesi iliyofunguliwa na ndugu wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa
Geita, Alphonce Mawazo wakipinga zuio la polisi kuchukua na kuaga mwili
wa Mawazo kwa maelezo ya kuwepo kwa mlipuko wa ugonjwa wa Kipindupindu.
Baba
mdogo wa Mawazo, Mchungaji Charles Rugiko alifungua kesi hiyo juzi
kutokana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Charles Mkumbo kupiga
marufuku shughuli za kuaga mwili wa marehemu aliyeuawa na watu
wanaodaiwa ni wafuasi wa CCM Novemba 14.
Usikilizaji wa kesi hiyo
uliochukua saa tatu kutokana na uwapo wa mvutano wa kisheria kwa
mawakili wa pande mbili, ilianza kusikilizwa saa 5:00 asubuhi hadi saba
adhuhuri na Jaji Lameck Mlacha.
Kesi hiyo namba 11 ya mwaka 2015, iliyovuta hisia za watu wengi jijini Mwanza, mlalamikaji anaomba mahakama
kuondoa zuio la Polisi kuzuia kuagwa mwili wa Mawazo; Kutoa tamko la
zuio la RPC kuwa ni batili na kinyume cha sheria na mahakama imkataze
Kamanda Mkumbo kujihusisha na shughuli za mazishi na kuaga mwili huo.
Note: Only a member of this blog may post a comment.