Richard bukos
MASTAA wa Bongo, Idriss Sultan na Wema Sepetu,
Alhamisi iliyopita walikuwa kwenye Ikulu ya Rais wa Awamu ya Tano wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli wakionesha
mahaba yao hadharani.
Mastaa hao ambao mara kadhaa wamekuwa wakikanusha vikali kuwa na
uhusiano wa kujifunika shuka moja lakini mapozi yao ndiyo yalisababisha
wawe gumzo ndani ya ikulu hiyo iliyopo Magogoni jijini Dar ambapo
kulikuwa na hafla ya kumpongeza rais huyo baada ya kuapishwa.
Katika tukio hilo wawili hao bila soni walionekana kuzunguuka kwenye
viwanja vya ikulu hiyo wakiwa wamekumbatiana kama bibi na bwana hali
iliyozidi kukoleza minong’ono kwenye viwanja hivyo.
“Pliiiz paparazi naomba hebu tuache jamani kwa kushikana hivi wewe
umekutafsiri vipi, mbona ni kawaida tu, huyu mimi ni rafiki yangu
namheshimu sana,” alisema Wema.

Note: Only a member of this blog may post a comment.