JAMANI! Siku chache tu kufuatia Jeshi la Polisi
Tanzania kupitia msemaji wake, Advera Bulimba kupiga marufuku maandamano
na mikusanyiko ya kisiasa nchini kote kwa hofu ya kutokea kwa uvunjifu
wa amani, kijana mmoja (jina halikupatikana mara moja) anashikiliwa na
Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kwa madai ya kunaswa na mabomu 10
kinyume cha sheria.
ILIKUWA SAFARI YA DAR
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha ndani ya jeshi hilo mkoani Shinyanga,
kijana huyo ambaye pia ni mfanyabiashara wa madini, alikamatwa usiku wa
Novemba 5, mwaka huu nyumbani kwa baba yake mzazi mjini Kahama ikidaiwa
kwamba alikuwa katika mchakato wa safiri ya jijini Dar na mabomu hayo.
CHANZO NI RAIA WEMA
CHANZO NI RAIA WEMA
“Polisi walipewa taarifa na raia wema. Wakaenda nyumbani kwa baba
yake ambako kweli walimnasa akiwa na mabomu hayo kumi. Hii hali imezua
maswali mengi! Baadhi ya watu wanahisi Dar ilikuwa kituo cha kupita tu,
huenda alikuwa akienda nje ya nchi, wengine wanasema Dar ndiyo kilikuwa
kituo chake kikuu.
“Lakini walimkamata, wakampeleka polisi na mabomu yake yote. Unajua
hakuna kipindi ambacho Jeshi la Polisi Tanzania liko macho kama sasa.
Lengo kubwa ni kulinda amani ya nchi, hususan baada ya uchaguzi mkuu
kupita ambapo baadhi ya watu walionesha ishara ya kutaka kuvunja amani
na kuleta vurugu,” kilisema chanzo hicho.
Kufuatia tukio hilo, baadhi ya wananchi mjini Kahama wamelitaka jeshi
la polisi kuzidisha ulinzi na upelelezi ili kuwabaini watu wanaoweza
kumiliki zana za kijeshi kinyume cha sheria hasa katika kipindi hiki
ambacho, nchi imekuwa katika mapito ya uchaguzi.
“Kwa sasa jeshi la polisi si la hapa Kahama au Shinyanga tu, nchi nzima lazima liwe makini sana.
Kuna watu wanataka kuvunja amani. Lakini kuna watu tunapenda amani,” alisema Chubwa Pomongo, mkazi wa Kahama.
WIKIENDA LAMSAKA RPC
Kuna watu wanataka kuvunja amani. Lakini kuna watu tunapenda amani,” alisema Chubwa Pomongo, mkazi wa Kahama.
WIKIENDA LAMSAKA RPC
Juzi, kwa njia ya simu, gazeti hili lilimsaka Kamanda wa Polisi Mkoa
wa Shinyanga, SACP Justus Kamugisha na kumuuliza kuwepo kwa madai ya
kijana huyo kukamatwa ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Ni kweli.
Alhamisi iliyopita, majira ya usiku hivi, Jeshi la Polisi Mkoa wa
Shinyanga lilimkamata huyo mtu akiwa na mabomu kumi (10) na ditoneta (za
kusababisha mlipuko) elfu tano (5,000).
“Mtu huyo anajishughulisha na biashara ya madini katika mgodi mdogo
wa Ilalo, Geita. Bado tunamshikilia kwa vile uchunguzi unaendelea ili
kujua lengo la yeye kuwa na mabomu hayo kumi na ditoneta elfu tano ni
nini.”
Kamanda Kamugisha alipoulizwa jina la mtuhumiwa huyo, alisema mpaka afike ofisini kwake kwa vile alikuwa nje ya ofisi kwa siku hiyo ya Jumamosi.
Kamanda Kamugisha alipoulizwa jina la mtuhumiwa huyo, alisema mpaka afike ofisini kwake kwa vile alikuwa nje ya ofisi kwa siku hiyo ya Jumamosi.
Mfano wa mabomu ambayo yamekamatwa kutoka kwa kijana huyo.
DCI DIWANI
Pia, Wikienda lilimtafuta Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai Tanzania
(DCI), Diwani Athuman Msuya kwa lengo la kusikia kauli yake kuhusiana na
tukio hilo lakini simu yake iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa.
TUJIKUMBUSHE
Mwishoni mwa wiki iliyopita jeshi la polisi nchini lilipiga marufuku ombi la maandamano la baadhi ya vyama vya siasa nchini baada ya uchunguzi wake kubaini kuwepo na mihemko ya kisiasa ndani ya jamii inayoweza kusababisha uvunjifu wa amani.

Kutokana na hali hiyo, jeshi hilo lilisema litaendelea kushikilia
msimamo wake wa awali wa kuzuia mikutano na maandamano yoyote mpaka hali
itakapotengemaa.
Kauli ya jeshi hilo imefuatia baada ya baadhi ya vyama vya siasa kuwasilisha ombi la kufanya mikutano ya hadhara na maandamano nchi nzima huku vyama vingine vikitaka kufanya maandamano yasiyo na ukomo.
Kufuatia hali hiyo jeshi hilo limewataka wananchi kushirikiana na jeshi la polisi ili kudhibiti hali hiyo huku likivitaka vyama vya siasa kufuata sheria na kutii ili kuepusha vurugu zisizo na ulazima.

Note: Only a member of this blog may post a comment.