Tuesday, November 10, 2015

Anonymous

Maamuzi ya Jeshi la Polisi Baada ya Huyu Askari wa Tanga Kunaswa Kwenye VIDEO Akifanya Yake!


Novemba 9, 2015 kulikuwa na headlines kwenye mitandao mbalimbali baada ya video kusambazwa na wasiojulikana ikimuonyesha Askari wa usalama wa barabarani Anthony Temu kutoka kituo cha polisi Kabuku Tanga akichukua rushwa kutoka kwenye gari alilolisimamisha.

Baada ya hii taarifa kusambazwa mitandaoni kamanda wa polisi mkoani Tanga, Zuberi Mwombeji amethibitisha hii ishu nzima kutokea na kwamba Temu alihojiwa na kukiri kwamba ni kweli alifanya hivyo, baada ya hapo Kamanda Mwombeji amesema wamemkabidhi kwa TAKUKURU.

Moja ya picha kutoka kwenye hiyo video iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii.
‘Tumechunguza taarifa zile na tumemtafuta tumemshughulikia na kumkabidhi kwa maafisa wa TAKUKURU wanaendelea na uchunguzi sababu wao ndio wanashughulika na maswala haya ya rushwa‘ – Kamanda Mwombeji.
Hapa chini nimekuwekea sauti. Sikiliza live ilivyokua hapa.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.