
MTU mwenye
tatizo la kutoshika mimba kitaalamu tunasema Infertility. Kwa mujibu wa
tafiti mbalimbali, wanandoa asilimia 50 wanapata mimba ikiwa
watajamiiana bila kutumia kinga wakifanya tendo hilo ndani ya miezi
mitatu na asilimia 75 baada ya miezi sita na asilimia 95 baada ya mwaka
mmoja.
Sababu za tatizo la kutopata mimba ni nyingi sana na baadhi yake ni hizi zifuatazo:
Matatizo ya mbegu za kiume (Sperm Disorders). Asilimia 35 ya wanaume wana tatizo hili na lingine ni kutopevuka kwa mayai kwa wanawake yaani kitaalamu Ovalatory Dysfunction, asilimia 20.
Matatizo mengine ni yale yasiyo ya kawaida ya ute wa shingo ya uzazi ambapo ni asilimia 5 tu. Wengine huwa na matatizo ya homoni na wapo ambao hawapati mimba na sababu zao hazijulikani ni asilimia 10. Wengine ni kutokana na kuwa na msongo na wasiwasi.
Tatizo lingine la kutoshika mimba husababishwa na hitilafu katika mirija ya uzazi (Tubal Dysfunction), hawa huwa asilimia 30.
Sababu zote hizi nitaeleza mojamoja kwa kirefu katika matoleo yetu yajayo lakini wote wenye tatizo hili wanashauriwa kuhudhuria kliniki za akina mama ili waonane na madaktari.
Lakini pia wanashauriwa kufuatilia siku zao za mzunguko wa hedhi na tendo la ndoa mara kwa mara hasa baada ya siku 10 kutoka siku anamaliza hedhi na aanzie siku ya kwanza ya kupata hedhi.
Wanawake wanashauriwa wawe wanapima joto la mwili asubuhi na jioni kipindi cha kushika mimba na kama litaongezeka kwa nyuzi joto 0.5 wanashauriwa kipindi hicho kufanya tendo la ndoa.
Kwa nchi za Ulaya na Marekani wana kipimo cha kuonesha siku ambayo yai litapevuka, hivyo mtu kuwa na uhakika na siku ya kupata mimba akiamua.
Kipimo hicho kinaitwa Luteinizing Hormone Prediction Test Kits. Wanawake wanaotaka kupata mimba wanashauriwa kuepuka ulevi na uvutaji wa sigara wa kupindukia. Lakini hata wale wenye mimba wanashauriwa kuepuka vitu hivyo.
Tatizo la mwanamke kutoshika mimba limegawanyika katika makundi mawili. La kwanza huitwa kitaalamu ‘Primary Infertility’.
Kundi hili ni lile ambalo mwanamke hajawahi kushika mimba hata siku moja na kundi la pili huitwa ‘Secondary Infertility’. Hili ni lile la wanawake ambao wamewahi kushika mimba wakajifungua au mimba zikaharibika.
Zipo sababu nyingi zinazofanya. Itaendelea wiki ijayo.
Note: Only a member of this blog may post a comment.