Wednesday, November 25, 2015

Anonymous

Kinachoongelewa na Wakenya Baada ya Rais Wao, UHURU KUNYATTA Kuvunja Baraza la Mawaziri!

Siku moja baada ya Rais wa Tanzania kuweka headlines kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter kwa raia wa Kenya, Rais Uhuru Kenyatta ameingia kwenye headlines za aina hiyo baada ya kufanya mabadiliko katika Baraza la Mawaziri la Kenya kwa kuchukuwa maamuzi ya kuwapiga chini Mawaziri wote ambao Wizara zao zinakumbwa na kashfa nzito za ufisadi!
Kama ilikuwa haijakufikia mpaka muda huu basi ikufikie kuwa uamuzi wa Rais Uhuru Kenyatta umekuja siku moja baada ya kutangaza kuwa tatizo la ufisadi Kenya ni tishio kubwa kwa kitaifa hilo na kuahidi kufanya mabadiliko hivi karibuni kama Rais anayeshikilia ofisi.
UHURU2
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta.
Vitu vimetendeka, na baadhi ya maamuzi yaliyofanywa na Rais Uhuru Kenyatta siku ya jana ni pamoja na kuongeza idadi ya Wiazara kutoka Wizara 19 hadi Wizara 20 kwa kile alichodai kuwa ni kuzisaidia Wizara kutekeleza majukumu yao kwa ubora zaidi pamoja na kufanya uchaguzi mdogo ndani ya Wizara hizo.
Mawaziri waliokumbwa na kashfa za ufisadi walijiondoa kwenye Wizara zao na sasa wanakabiliwa na kesi za kujibu Mahakamani huku wengine kama Waziri wa Ugatuzi, Anne Waiguru alijiondoa madarakani kutokana na kashfa zilizoweka headlines kubwa Kenya, za kununua kalamu ya moja ya BIC kwa zaidi ya Tzs. 200,000/- za Kitanzania!
UHURU3
Anne Waiguru aliyekuwa Waziri wa Ugatuzi, Kenya.
Maamuzi haya ya Rais Uhuru Kenyatta yameibua mjadala mkubwa kwa Wakenya na kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter, baadhi wakionekana kufuraishwa na kitendo hicho, huku wengine wakihoji maamuzi ya Rais wao.
Nimefanikiwa kuzinasa baadhi ya hizi tweets za Wakenya kwenye Twitter na kuziweka hapa chini…
UHURU1
>>> “Je, makatibu wa wizara wanasainishwa mikataba ya utendaji? Hiyo iliyofutwa waliitendea kazi? Je ilihojiwa? #CabinetReshuffle“. <<< @BonifaceMwangi.
UHURU2
 >>> “Baada ya kuthibitisha chuki yake dhidi ya wanafunzi wa shule za Kenya, #Kaimenyi  sasa anaende akapambane na Wizara ya Ardhi ambayo tayari imeshavurugwa #CabinetReshuffle“. <<< @MugandaClay.
UHURU4>>> “Kaimenyi ilitakiwa arudishwe kwao… Maji yakichafuka unayamwaga, hubadilishi kikombe“. <<< @TheDanMuniu.
UHURU5
>>> “#CabinetReshuffle kwanini tunawateua Wabunge na Senetors? Kwa ajili ya uchaguzi mdogo? Kwanini Mh. Rais?” <<< @EvansAgaya.
UHURU6
>>> “Sikudhani kuwa Serikali yetu ingepata uafadhali lakini #CabinetReshuffle inatokea na kazi zinaanza. Yay! Mifuko mengine ya kujaza“. <<< @RuthChelimo.
UHURU7
 >>> “Kuongezeka kwa nafasi za Baraza la Mawaziri na uchaguzi mdogo utakao gharimu mamilioni. Utafurahishwa na jinsi tunvyofikiria #CabinetReshuffle“. <<< @KenyaWest.
UHURU8
 >>> “#CabinetShuffle Michezo, Utamaduni na Sanaa… Hassan Wario. Kwahiyo biashara ya kawaida inaendelea!” <<< @CarolRadull.
UHURU9
 >>> “Kwa jinsi #HarambeeStars walivyofanyiwa, @UKenyatta bado anatupatia #HassanWario kweli?? Nadhani ningefanya vizuri zaidi #CabinetReshuffle“. <<< @PhannuelPhanntastic.
UHURU10
>>> “Nina matumaini na #CabinetReshuffle mpya, kikwazo kikubwa ni #Wario kwenye michezo. Harambee Stars ilikuwa mchezo wa kuigiza sasa Riadha utakuwa mchezo wa kuigiza“. <<< @LotanSalapei.
Kama ilikupita, hapa chini ipo full video ya Hotuba ya Rais Uhuru Kenyatta kuhusiana na maamuzi yake ya kulivunja Baraza la Mawaziri la Kenya.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.