SIJALI!
Mrembo mmoja mkazi wa mjini Tunduma wilayani Momba mkoani hapa ambaye
jina lake halikuweza kufahamika mara moja amejikuta akiwa sinema ya bure
kufuatia uamuzi wake wa kujitosa kwenye maji yenye tope akidai
anasherehekea ushindi wa Rais Mteule wa Awamu ya Tano, Dk. John Pombe
Magufuli wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mrembo huyo akijigaragaza kwenye matope.
Tukio hilo la aina yake lilijiri hivi karibuni maeneo ya Mtaa wa CCM mjini hapa ambapo wanachama wa chama hicho walikodi muziki na kushangilia ushindi huo.
Baadhi ya wanachama wa chama hicho walipozungumza na gazeti hili
walisema mkazi huyo ni shabiki mkubwa wa chama hicho na alikuwa
akiwatania wanachama wa vyama vya upinzani kuwa, wataweza kukitoa chama
hicho kwenye udiwani na ubunge, lakini siyo urais.
Hivyo,
ushindi wa Magufuli ulisababisha mkazi huyo kuwa na furaha ya
kupitiliza huku akiwa amegida ulabu kwa ajili ya kushangilia. Mbaya
zaidi huku mvua ikinyesha kwa mbali, alijitupa ndani ya tope na
kuendelea kucheza muziki.
Mrembo huyo akijigaragaza kwenye matope.
Tukio hilo la aina yake lilijiri hivi karibuni maeneo ya Mtaa wa CCM mjini hapa ambapo wanachama wa chama hicho walikodi muziki na kushangilia ushindi huo.

Note: Only a member of this blog may post a comment.