Leo
mpenzi msomaji wa safu hii, nimekuja na mada mpya ambayo imenisukuma
kuwaandikia wanandoa na wapenzi walioko kwenye uhusiano kwa muda mrefu
kwani wengi hujikuta wameachwa na kuona kuwa ni ghafla kumbe
hawakutambua kwa kujua ni utani.
Kauli anazozitoa mwanaume wako ni wazi kabisa kuwa amekuchoka wengi hawazitambui sasa zisome kwa makini na uzielewe.
Tukiachana sisi si wa kwanza Kauli kama hii mwanaume hawezi kukuambia mkiwa kwenye mapenzi kwa mara ya kwanza, hivyo ni lazima kwa kukutamkia hivyo ujue moja kwa moja umechokwa.
Hivi ni nani ambaye hajui kuwa mapenzi ni malumbano ya mara kwa mara hata kwa vitu vidogo? Kama hampendani hamuwezi kutofautiana kwani mtakutana wapi au mtakutanishwa na nani hasa?
Ulipoingia kwenye penzi kwa mara ya kwanza hata alipokuwa akikukwaza uliomba yaishe mapema na wala hukuwahi kufikiria kukwambia kuwa tukiachana sisi si wa kwanza, ulitumia nafasi yako kikamilifu kwa kumbembeleza na akakuelewa mkamaliza mzozo.
Ipo siku utajutia hili penzi
Maana yake nini? Mpaka mnafikia hatua anakwambia hivyo ni wazi anashindwa kujitoa lakini pia anao uwezo wa kujitoa hivyo anakuandaa kisaikolojia.Kwa mtu unayempenda kwa dhati huwezi kumwambia ipo siku atajutia penzi ni neno lisilostahili kwa mpenzi wako, ukiona unaambiwa hivyo jua siku zako zinahesabika.
Afu we mwanamke una mdomo sana
Ukiona mpenzi wako anakerwa na
mdomo wako mara kwa mara na anakutamkia jua wazi mapenzi hakuna. Wanaume
wengi hawapendi mwanamke anayeongea hasa kama anamkosoa kwa jambo
fulani.
Mfano kama kuna vitu ulikuwa ukimwambia mwanzo anakubali na kuendana na wewe lakini akishakuchoka ukiongea tu anakuona kero, hii pia ni dalili ya kuachwa.
Kwani nilikukuta mtoto, tumejuana ukubwani
Wanaume wengi wanapenda kutumia kauli hii pale wanapowachoka wapenzi wao hasa wanapokuwa kwenye malumbano, bila shaka msomaji utakuwa na ushahidi wa hili hasa kwa wale waliowahi kukutana na maneno haya wataniunga mkono.
Ni maneno yanayouma na kujirudia kwenye ubongo wa mwanamke pia hupunguza mapenzi kwani mwanamke akitamkiwa hivyo mara kwa mara hujikuta ubongo unaanza kukubali na kupunguza mapenzi kwa yule aliyekuwa akimpenda.
Kwa wanaume wote
Kama bado unampenda mpenzi/mkeo kamwe usimtamkie maneno haya ni sumu kubwa, huenda unatamka kwa bahati mbaya unapokuwa na jazba lakini yamekuwa yakiwaumiza wenza wenu na wakiamua kuachana nanyi watawachukia milele.

Note: Only a member of this blog may post a comment.