HATIMAYE MABASI YA MWENDO KASI KUANZA KAZI RASMI MWEZI DESEMBA JIJINI DAR
Mabasi ya mwendokasi yatakayofanya kazi eneo la Morogoro Road kuanzia Kimara mpaka Kivukoni jijini Dar es Salaam.
Mabasi hayo wakati yanawasili Bandarini jijini Dar.
Mkurugenzi mkuu wa wa mradi wa mabasi yaendayo kasi UDA-RT, Bw. Robert Kisena ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Usafiri Dar es Salaam amesema
mabasi ya mwendokasi yataanza kufanya kazi rasmi mwezi Desemba kwenye
Barabara ya Morogoro kuanzia Kimara mpaka Kivukoni.
Mabasi hayo tayari yameshawasili hapa nchini, kitu
kilichobakia ni kuweka mfumo wa kieletroniki utakaokuwa unajiendesha
wenyewe wa kulipa nauli kwa abiria.
Amesema
pia tani kumi ya mageti yatakayowekwa kwenye sehemu abiria
watakapopandia mabasi hayo, yamewasili nchini jumatano ijayo, yataanza
kufungwa siku yoyote na ujenzi huo utamalizika ndani ya wiki tatu.
Mpaka
sasa UDA-RT imepokea mabasi 140, mabasi 101 kati ya hayo yana uwezo wa
kubeba abiria 150, yaliyobaki yana uwezo wa kubeba abiria 80 tu. Mradi huo utasaidia na kurahisisha adha ya usafiri Jijini Dar.
USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK
TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)
Note: Only a member of this blog may post a comment.