Njemba huyo akionekana kurandaranda kwenye Maduka ya Mlimani City.
Boniphace Ngumije na Brighton Masalu
Taharuki!
Katika hali ya kushtua, njemba mmoja mtata mwenye asili ya Kiarabu
amezua tafrani kwenye Maduka ya Mlimani City yaliyopo Barabara ya Sam
Nujoma, jijini Dar baada ya kudakwa akitalii na kupiga picha za mnato
kwenye maeneo maalum bila kujulikana lengo lake.
…Akikatiza kwenye vikordo
Kwa mujibu wa shuhuda wetu, sekeseke
hilo lilijiri kwenye maduka hayo mapema wiki hii, majira ya mchana
ambapo jamaa huyo aliyekuwa na ‘mandevu mengi na marefu’ alitinga mahali
hapo huku akiwa amevalia mavazi meusi tii.
Akiwa kwenye korido za maduka hayo, mtu
huyo alianza shughuli ya upigaji picha aliyokuwa anaifanya kwa tahadhari
kubwa kwa kutumia kifaa maalum chenye umbile la kamera za dijitali.
“Jamaa alikuwa akizunguka sehemu maalum
alizopanga kuzifanyia kazi bila kuogopa sheria ambazo haziruhusu mtu
kupiga picha maeneo hayo.
Kwa mbali akitokomea chooni.
“Baadaye alitiliwa shaka kutokana na watu kuingiwa hofu juu yake kwani baadhi walikuwa wanamkimbia ndipo akadakwa na walinzi.
“Walinzi wa Mlimani City walipomkamata
walimhoji kwa nini anapiga picha, akasema alikuwa analinganisha uzuri wa
maduka hayo na huko kwao alikotoka,”alisema shuhuda.
Baada
ya kuudaka ubuyu huo, timu ya waandishi wetu iliingia kazini na
kuelekea moja kwa moja Mlimani City kuzungumza na Meneja Mkuu wa maduka
hayo, Pastory Mrosso ambaye alisema:
“Ni kweli tukio hilo limetokea lakini
lilikuwa ndani ya uwezo wetu wa vyombo vya usalama tulivyonavyo maana
jamaa hakuchukua muda mrefu kufanya hivyo, alikamatwa na kuhojiwa.
Baadaye aliamuriwa kuzifuta picha hizo kisha aliachiwa huru.”
Note: Only a member of this blog may post a comment.