Kha! Dada wa mkali wa Bongo Fleva,
Nasibu Abdul ‘Diamond, Mwajuma Abdul ‘Queen Darleen’, amefanyiwa kitu
mbaya na baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki baada ya kumwagiwa maji,
pombe, soda na mchanga huku wengine wakimpaka matope mwilini.
Ilielezwa kwamba baada ya kila kitu
kukamilika na muda kutimia, Mwengi alimdanganya Queen Darleen kuwa kuna
kitu anataka wakachukue kwenye ofisi hiyo ambapo mrembo huyo alikubali.
Kufuatia hali hiyo, Queen Darleen alijikuta akiangua kilio kama mtoto
huku akiwaomba wamsamehe kwani alikuwa
anaumwa lakini ombi lake halikuzingatiwa kwani waliendelea ‘kumsulubu’
kiasi cha kuishiwa nguvu na kujikuta akilala chini akiwa hoi.
Hata hivyo, walipoona anaweza kupata mshtuko au kuzimia, walimuacha na kuanza kumuimbia ‘happy birthday to you’, jambo lililomshtua na kuanza kumlaumu Mwengi kwa kutomjulisha mapema kwani angeweza kupoteza maisha kutokana na mshtuko alioupata.

Akizungumzia tukio hilo, Queen Darleen ambaye ni msanii wa Bongo Fleva aliliambia gazeti hili kuwa katika maisha yake hakuwahi kufanyiwa sapraizi kubwa kama hiyo wala kumwagiwa maji kiasi kile hivyo aliwashukuru wote waliokumbuka siku yake hiyo muhimu.

Note: Only a member of this blog may post a comment.