Thursday, October 8, 2015

Anonymous

Wako Wapi Wabunge Washangiliaji wa LOWASSA na Wenyeviti Watiifu Kwake?

Siku Rais Jakaya Kikwete alipolihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kulitaja jina la Edward Lowassa wabunge walilipuka kwa kushangilia na Bunge kuzizima. Rais Kikwete alikuwa akihitimisha miaka ya Bunge kuelekea kufanyika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu. Jina la Edward Lowassa lilitajwa wakati Rais Kikwete akiwataja Mawaziri wakuu aliofanya nao kazi na kuwashukuru.
Kulipuka kwa Bunge kulimaanisha kuwa Edward Lowassa alikuwa akiungwa mkono na wabunge wengi ambao wengi wao wanagombea tena. Lakini wengi wamebaki CCM baada ya Lowassa kuhamia CHADEMA. Kwakuwa wakati huo hata mchakato wa kura ndani ya CCM haukuwa tayari, nguvu ya Lowassa ilijidhihirisha hata mbele ya Rais Kikwete. Mara nyingine ilikuwa ni kule Dodoma wakati wimbo wa Lowassa ulipoimbwa baada ya kukatwa jina.

Pia, walijitokeza wenyeviti wa mikoa na hata makada kindakindaki wa CCM waliojipambanua kama wanaomuunga mkono Lowassa wakati akiwa CCM. Ingawa wapo waliojitoa CCM na kujiunga na CHADEMA kumfuata Lowassa, wabunge wengi waliomshangilia na wale wenyeviti waliomuunga mkono wamebaki CCM wakiwa kimya. Wako wapi waendelee kumuunga mkono chaguo lao? Nini kimempata Msukuma na Kangi Lugora? Ni waoga au bendera-fuata upepo? Waaminike?
By Petro E. Mselewa; JF

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.