Friday, October 9, 2015

Anonymous

VIDEO: Mume Amburuza Mkewe Mjamzito Barabarani na Gari Bila Huruma!

Tukio hili limetokea huko Texas,Marekani baada ya ugomvi kati ya mume na mke ambapo mama mwenye ujauzito wa miezi nane alijikuta akihatarisha maisha yake baada ya mume wake kumburuza kwa gari bila kujali hali yake.

Tukio hilo la kushangaza lilitokea baada ya wawili hao kugombana ambapo mama huyo alijikuta akiburuzwa na mumewe huyo bila huruma.

Kilichotokea ni kwamba mama huyo alimkuta mumewe ndani ya gari katika eneo la kupaki magari akiwa na mwanamke mwingine na katika kubishana akaamua kuondoa gari kwa hasira huku mke wake akiwa mbele ya gari.

Kamera za waandishi wa habari hazikuwa nyuma kurecord tukio hilo ambapo mama huyo aliponea kupoteza maisha na kupata majeraha ya kawaida baada ya kuokolewa na msamaria mwema.
Mume wa mama huyo Escobedo, aliwekwa mikononi mwa Polisi masaa machache baada ya tukio hilo
Cheki tukio lenyewe lilivyokuwa hapa

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.