Friday, October 9, 2015

Anonymous

Kingunge vs. CCM, Dk. Slaa kwa Magufuli, Rais wa Nigeria na Uchaguzi Tz? Kagame? Nchemba je? (Audio)

Asubuhi ya kila siku lazima ianze na uchambuzi wa magazeti redioni @CloudsFM, pengine ulikuwa kwenye foleni na nyingi zimekupita na kama kuna moja uliikosa basi karibu uperuzi na hizi nyingine kufidia. 

Kingunge azidi kuipasua CCM, Dk. Slaa asema Magufuli ndio chaguo sahihi, Lowassa avunja rekodi ArushaRais wa Nigeria kusimamia Uchaguzi Mkuu October 25!? 

Marais wastaafu wa Nigeria Goodluck Jonathan na wa Msumbiji Almado Emilio Guebuza wanatarajia kuja kuongoza jopo la waangalizi wa Kimataifa wakati wa Uchaguzi Mkuu October 25 wakiwa miongoni wa waangalizi 600 kutoka umoja wa EUDk. John Magufuli ampigia debe Mrema Mkoa wa Kilimanjaro asema kuwa itakuwa ni dhambi kumchagua mtu ambae haijui vizuri historia ya jimbo la Vunjo kama yeye. 

Kingunge apanda jukwaa la UKAWA kumnadi mgombea Urais kupitia CHADEMA Edward Lowassa Arusha, aishambulia CCM asema haitoweza kuiongoza Serikali kwa awamu ya tano… Mchungaji Christopher Mtikila amezikwa jana katika kijiji cha Milo mkoani Njombe. 

Mgombea Ubunge Bunda Mjini kupitia CHADEMA Esther Bulaya alazwa mahabusu mjini Bunda kwa madai yakuwa yeye na wenzake walitaka kuvamia kituo cha Polisi, Mgombea huyo na wenzake kufikishwa Mahakamani leo. 

Mwigulu Nchemba amewaonya watu wanaotumia vibaya maneno ya Baba wa Taifa Mwl. Julius K. Nyerere, Mahakama yamsafishia njia Rais Paul Kagame na sasa kutawala kwa awamu ya tatu.
Kusikiliza uchambuzi wote wa magazeti kwenye #PowerBreakfast bonyeza play hapa chini.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.