Ligi Kuu Uingereza
imeendelea kwa michezo kadhaa kupigwa katika viwanja tofauti tofauti,
miongoni mwa michezo iliyokuwa inapewa nafasi kubwa au kuteka hisia za
mashabiki wengi wa soka ni mechi kati ya Arsenal dhidi ya Everton, mchezo ambao umepigwa katika dimba la Emirates.
Arsenal ambao
wanafundishwa na kocha wa Kifaransa aliyedumu na klabu hiyo kwa zaidi ya
miaka 10 wamefanikiwa kupata ushindi katika uwanja wao wa nyumbani,
ushindi ambao umewafanya Arsenal kutimiza jumla ya point 22 na kushika nafasi ya kwanza katika msimamo wa Ligi.
Timu ya Arsenal imefanikiwa kushinda kwa jumla ya goli 2-1, magoli ambayo yalifungwa na Olivier Giroud kwa kichwa dakika ya 36 kabla ya dakika mbili mbele beki wa klabu hiyo Laurent Koscielny kupachika goli la pili, kwa upande wa Everton walipata goli la kufutia machozi kupitia kwa Ross Barkley dakika ya 44 ya mchezo.
Video ya magoli ya mechi ya Arsenal Vs Everton
Video ya magoli ya West Ham United Vs Chelsea

Note: Only a member of this blog may post a comment.