Mgombea Ubinge wa jimbo la Ilemela kwa tiketi ya Chadema, Highnes Kiwia
Kiwia amesema kuwa matokeo yaliyompa ushindi Mabula yalikuwa ni ya kutengenezwa ili kumbeba mgombea huyo wa CCM kabla ya kufanyika kwa uchaguzi.Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kiwia amesema atatumia haki ya kikatiba kupinga matokeo hayo mahakamani ili maoni ya wananchi kuheshimiwa na kupata haki zao za msingi.
Hata hivyo katika matokeo hayo, msimamizi wa uchaguzi huo, John Wanga, alimtangaza Angelina Mabula mshindi kwa kura 81, 424 dhidi ya Kiwia aliyepata kura 61,679.
Kiwia pia amesema kuwa katika baadhi ya vituo majina ya wapiga kura yaliongezwa, mawakala wake kutishiwa na baadhi ya wafuasi wa CCM kitendo ambacho dhahili alidai uchaguzi haukuwa huru.
“Matokeo haya yalikuwa yamepangwa kabla ya uchaguzi kufanyika, tunaenda mahakani kupinga matokeo haya, hatutaona maoni ya wananchi yanapotea,” amesema Kiwia.
Pia Kiwia alivitaja baadhi ya vituo ambavyo vilikuwa na kasoro kuwa ni pamoja na Kitangiri, Ilemela na Nyansaka na kwamba wamejipanga muda wowote kwenda mahakamani. Kwa upande wake Kiongozi wa Chadema, Kanda ya Ziwa Victoria, Tungaraza Njugu amesema matokeo ya uchaguzi huo sio sahihi na kwamba maoni ya wananchi walio wengi yamepora na CCM
Note: Only a member of this blog may post a comment.