Monday, October 5, 2015

Anonymous

Ushindi wa Goli 5-2 Ukakamilishwa na Jamaa Kumvalisha Pete Mchumba Wake Hapo Hapo Uwanjani… (+VIDEO)

Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Nigeria Super Eagles, John Ogu ameteka hisia za mashabiki wake baada ya kuamua kumvalisha pete ya uchumba mpenzi wake wa siku nyingi Adaolisa. 

Ogu anayecheza soka la kulipwa huko Israel katika klabu ya  Hapoel Be’er Sheva alifanya tendo hilo baada ya kumalizika kwa mchezo wao dhidi ya Maccabi Peteh ambapo waliondoka na ushindi wa mabao 5-2. 

Mshambuliaji huyo alimwomba refa apulize filimbi kabla ya kumwita mpenzi wake katikati ya uwanja kisha akapiga goti na kumvalisha pete huku akishangiliwa na wachezaji wenzake.
Video iko hapa mtu wangu…

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.