Monday, October 26, 2015

Anonymous

UPDATES: Matokeo Rasmi ya URAIS Usiku Huu Kwa Majimbo Mengine 14 Yatangazwa....MAGUFULI Bado Anaongoza

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Usiku huu imeendelea kutoa matokeo ya awali ya urais katika majimbo 27 ambapo mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk John Magufuli anaongoza kwa majimbo 17 wakati Mgombea wa Chadema, Edward Lowassa anaongoza majimbo 10.


Matokeo hayo yametangazwa na Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Mstaafu Damian Lubuva kwa awamu tatu, ambapo asubuhi  mwenyekiti huyo alitangaza majimbo matatu ambayo ni  Paje, Makunduchi na Lulindi ambayo yote Dk Magufuli ameongoza.

 

Majira ya alasiri , Jaji Lubuva alitangaza majimbo mengine 10 ambapo kati ya hayo majimbo sita yalionyesha Dk.Magufuli anaongoza huku majimbo manne yakionyesha Lowassa anaongoza.


Usiku  huu  majira  ya  saa  mbili , Jaji Lubuva ametangaza majimbo mengine 14 ambapo kati ya hayo majimbo 8 yalionyesha Dk.Magufuli anaongoza huku majimbo 6 yakionyesha Lowassa anaongoza.
Majimbo hayo ni kama  ifuatavyo: 
Matokeo ya Urais Singida Mjini

Kura: 56,558 

Magufuli (CCM): 36,035 

Edward Lowassa (Chadema): 19,007







Matokeo ya Urais Jimbo la Lindi Mjini   
Kura: 38,992  Magufuli (CCM): 21,088  Edward Lowassa(Chadema): 17,607 


Matokeo ya Urais Jimbo la Njombe Mjini   
Kura: 55,772   
Magufuli (CCM): 33,626   
Edward Lowassa(Chadema):20,368


Matokeo ya Urais Jimbo la Peramiho   
Kura:45,374   
Magufuli (CCM): 32,505   
Edward Lowassa (Chadema): 11,291


Matokeo ya Urais Jimbo la Mkinga   
Kura: 39,788   
Magufuli (CCM): 23,798   
Edward Lowassa (Chadema): 15,142


Matokeo ya Urais Jimbo la Moshi Mjini 
Kura:79,814 
Magufuli (CCM): 28,909  
Edward Lowassa (Chadema): 49,379


Matokeo ya Urais Jimbo la Nanyamba   
Kura: 44,437   
Magufuli (CCM): 24,904   
Edward Lowassa (Chadema): 16,992


Matokeo ya Urais Jimbo la Mbinga Mjini 
Kura: 42,717
Magufuli (CCM): 29,295   
Edward Lowassa (Chadema):11,695  

Matokeo ya Urais Jimbo la Kisarawe 
Kura: 38,012   
Magufuli (CCM): 24,086  
Edward Lowassa (Chadema): 13,093  

Matokeo ya Urais Jimbo la Mgogoni   
Kura: 7,539 
Magufuli(CCM):710   
Edward Lowassa (Chadema): 6,506  

Matokeo ya Urais Jimbo la Mtambwe   
Kura: 7,620   
Magufuli (CCM): 428 
Edward Lowassa (Chadema): 6,937
Jaji Lubuva amesema kuwa matokeo ya majimbo mengine ambayo yatakuwa tayari yatatolewa kesho  saa  tatu  asubuhi.
KAMA ‪HUKUCHEKI  MATOKEO YALIYOPITA===>>>INGIA HAPA!

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.