Thursday, October 8, 2015

Anonymous

UKAWA & Arusha, Magufuli & Mbowe, Kingunge kwa Lowassa?, Msigwa Mahakamani?#PowerBreakfast (Audio).

Asubuhi ya Alhamisi tarehe 8 October 2015 imeanza na uchambuzi wa magazeti redioni @CloudsFM The Peoples Station, na kazi yangu ni kuhakikisha zote kubwa za leo zinakufikia, kama hukuzipata zote, karibu uperuzi na hizi nyingine. 

UKAWA waingia kiwewe Arusha, Magufuli amgusa Mbowe kwao, Uganda wamtamani John Magufuli, Lowassa awasihi wananchi kukesha kulinda kura zao, TANESCO kumbeba Lowassa, Kingunge kumnadi Lowassa Arusha leo, PPRA yafichua madudu, Mama Salma Kikwete afunguka kuhusu Uchaguzi. 

Kampuni ya New Habari inayochapisha magazeti ya Mtanzania, Rai, Dimba, Bingwa na The African imelaani vikali uzushi, uongo na upotoshaji wa hali ya juu unaofanywa na watu wasio na nia njema na kampuni hiyo, wanaochapisha magazeti feki na kuyasambaza kwenye mitandao ya kijamii kwa nia ya kuichafua kampuni hiyo. 

Mgombea Ubunge CHADEMA jimbo la  Iringa, Mchungaji Peter Msigwa afikishwa Mahakamani na kupandishwa kizimbani kwa mashtaka manne moja ikiwa kushambulia Polisi, upelelezi juu ya kesi hiyo bado unaendelea. 

Mgombea Urais kupitia CHADEMA Edward Lowassa asema Serikali yake itaondoa ushuru wa mazao kwa wakulima ndani ya siku saba akiingia madarakani, Mgombea Urais wa CCM Dk. John Magufuli amesema anataka kuziba mirija ya ulaji kwa kukomesha mafisadi waliopo ndani ya CCM na vyama vingine. 

Tume ya Taifa na Uchaguzi NEC imewaagiza waratibu na wasimizi wa Uchaguzi pamoja na Makamanda wa Polisi kuhakikisha suala la ulinzi kwenye siku ya kupiga kura kwani usalama wa siku hiyo upo mikononi mwao huku ikiwaagiza waratibu, wasimamizi na maafisa Polisi kuhakikisha kuwa taratibu zote za kupiga kura zinafuatwa. 

Jaji Joseph Warioba asema msimamo wake kuhusu kuheshimiwa kwa maoni ya wananchi kuhusiana Rasimu ya Katiba mpya bado upo palepale, Mgombea Urais kupitia ACT Wazalendo, Mama Anna Mgwila asema akipata ridhaa ya kuwa Rais wa Tanzania atamchagua Dk. John Magufuli kuwa Waziri wa Ujenzi… Umoja wa Mataifa, UN yaridhishwa mwenendo wa maandalizi kuelekea Uchaguzi Mkuu October 25 wasema Tanzania ni mfano wa kuigwa kwa watu wengine.
Nimeirekodi pia sauti ya uchambuzi wote wa magazeti kwenye #PowerBreakfast na kuiweka hapa chini.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.