Geah Habib alifika nyumbani kwa Glory na kumkuta anasumbuliwa na ugonjwa wa kansa ambao matatibu yake ni ya gharama sana.
Amesimulia kwamba kansa yake imetokea sehemu ya haja kubwa..alianza kuugua njia ya haja kubwa kwa kuanza kujisikia maumivu makali na kutoka damu na vidonda hadi kushindwa kukaa, alipatiwa matibabu kwa muda wa miaka mitatu na alikua akipata nafuu lakini baada ya muda hali inarudi pale pale.
Glory anasema kabla ya kuanza kuumwa alikua akikaa hata wiki nne bila kupata choo na kumsababishia kupata maumivu makali kwa muda mrefu, baadaye alishauriwa kwenda hospitali ya Muhimbili na kuchukuliwa vipimo vikubwa ikiwemo kipimo cha kansa na kutakiwa kusubiri majibu.
Anasema kuna siku akiwa nyumbani alipigia simu na daktari kwenda kuchukua majibu yake na kutakiwa kwenda akiwa na ndugu zake, alipofika aliambiwa ana kansa.
Kwa sasa anahitaji msaada wa Watanzania ili aweze kupata kiasi cha milioni 25 ili akatibiwe India..
Msikilize Glory Swai akizungumza na Geah Habib hapa….

Note: Only a member of this blog may post a comment.