Tokea siku ile nilibadili mtazamo wangu juu yake kwa sababu kabla nilimuona ni fisadi na mtu asiyefaa kuwa kiongozi. Japo haindoi ukweli kuwa Lowassa ana uchafu wake na yeye lakini ni nani basi msafi amponde jiwe? Iwe ndani ya Chadema au CCM?
Pamoja na mambo yote aliyopitia nimependa ambavyo amekuwa na msimamo katika kusimamia lengo lake na hili ni moja ya sifa ambayo kiongozi anapaswa awe nayo. Kuna tofauti kati ya uchu wa madaraka na kutimiza ndoto na malengo uliyojiwekea. Uchu wa madaraka ni pale ambapo mtu amepewa dhamana ya uongozi kwa muda mrefu na bado anataka kuendelea hata kama wale ambao anawaongoza hawamtaki katika nafasi ile.
Lowassa aliutamani urais toka angali kijana hii ilikuwa ni ndoto yake. Aliutaka kwa ajili ya haya anayotuambia au kwa maslahi yake hilo jibu analo yeye na MUNGU pekee. Baada ya kushindwa 1995 walijiwekea mkakati na miaka 10 baadaye Lowassa alimuachia rafiki yake na akamsaidia mpaka akawa rais wa nchi hii, Lowassa alizawadiwa uwaziri mkuu kama njia ya kuja kushika majukumu ya Urais 2015. Hapo katikati yalipotokea ya kutokea na makubaliano yao yakaingia shimoni. Marafiki wakawa maadui wakubwa. Huku mmoja lengo lake likiwa ni kuwa rais wa nchi hii halijatimia. Rafiki yake alifanya kila jitihada kuhakikisha lengo na adhma ya rafiki yake haitimii.
Lowassa alifanikiwa, na Lowassa amegombea urais. Lowassa anadai ameibiwa kura kama madai yake yana ukweli mbele za MUNGU Lowassa ni Rais wa Nchi hii hata kama ataenda Monduli Kuchunga ng'ombe. Na kama basi ameshindwa kihalali basi Lowassa atakuwa ameshindwa kutimiza ndoto yake lakini ameshindwa dakika za mwisho katika kupigania ndoto zake. Hili ni funzo kubwa kwetu weka pembeni kashfa, mienendo na tabia zake binadamu wa aina yake ni wachache haswa kwenye nchi yetu.
Jipime mwenyewe ulipokuwa mtoto mdogo ulikuwa na ndoto ya kuwa nani ukiwa mkubwa? Je, leo unaiishi ndoto hiyo? Kama ndio hongera kwasababu wewe ni miongoni mwa wachache waliofanikiwa kuishi ndoto zao kama hapana ni ulikabili vipi changamoto zilizokufanya usitimize?.
Kama we ni mdogo basi jifunze na uchukue hatua kabla wakati haujakuacha.
Kama watanzania tunapaswa kujiuliza je, Rais mteule aliwahi kuota kuwa Rais alijiandaa na kupambana kufikia ndoto hii? Kama ni kwa bahati basi tutegemee nini? Na kama kweli alijiandaa na kupigania ndoto yake basi tutegemee nini kwa hili pia?!
-By Major Mwendwa
Note: Only a member of this blog may post a comment.