Saturday, October 31, 2015

Anonymous

Speed 120 Aliyoihaidi Mh. LOWASSA Ingetoka kwa Watu Hawa Kama Angeupata Urais

Edward Lowassa
Ni siku kadhaa zimeshapita ambazo watanzania wengi hasa wale wa mijini waliweka matumaini yao dhidi ya utawala mpya kama nilivyoelezea hapo juu...

Ilikuwa ukipita mitaani utagundua watu wakiwa katika matumaini mapya yenye furaha kuwa hakika yule watakayemchagua ndiye atapita lakini ikawa ndivyo sivyo.

Nilipopita mitaani hasa hapa Dar es salaam nilipata nafasi ya kusikia maoni ya watu wengi sana. Lakini moja ya maoni ya vijana wengi na wazee wengi pale ubungo kituo cha mabasi yaendayo mikoani ndiyo yaliyonikosha zaidi...

Ni pale niliposikia watu wakidadavua ile ahadi ya Lowassa ya speed 120 jinsi ambavyo angetekeleza chini ya baraza hili la mawaziri. Kijana mmoja niliyemfahamu kwa jina la Yassin alijaribu kuunda baraza la mawaziri chini ya Mh. Lowassa nalo lilikuwa hivi:
WAZIRI MKUU----Mh F.A. Mbowe

Waziri wa katiba na sheria---Mh. Tundu Lissu.

Waziri wa Maliasili na utalii---Mh. Rev Peter Msigwa

Waziri wa wanawake jinsia na watoto---Mh. Halima Mdee

Waziri wa ulinzi na usalama---Mh. G. Lema

Waziri wa mambo ya ndani----Mh. J J Mnyika

Waziri wa michezo na sanaa---Mh. Sugu

Waziri wa Waziri wa fedha---Mbatia

Waziri wa ardhi----Salumu Mwalimu

Aliendelea kushuka kushuka na akamaliza kwa kusema watanzania mnafikiri chini ya mawaziri hawa kwanini kusiwe na SPEED 120?

SASA: Leo nimepita tena mahali pale Ohooo...ndugu yangu watu kama wamemwagiwa maji....watu wamehuzunika saana watu hawana Amani wamepoteza matumaini hawana hili wala lile....ni sawa na mfungwa aliyewekwa gerezani kwa miaka zaidi ya hamsini baadaya sikuchache akitarajia kufunguliwa halafu siku hiyo anaambiwa ameongezewa miaka mitano tena....ohoooo....piga picha jinsi anatakavyoumia...basi ndivyo hali inavyoendelea huku mitaani....

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.