Mwigizaji wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja na staa wa Bongo Fleva, Abbott Charles ‘Quick Rocka’.
KWELI penzi ni kikohozi! Mwigizaji wa sinema za Kibongo, Kajala
Masanja na staa wa Bongo Fleva, Abbott Charles ‘Quick Rocka’ wamedaiwa
kuzama kwenye penzi zito licha ya wenyewe kutotaka watu wajue. Madai ya penzi hilo motomoto yameshereheshwa zaidi baada Quick kutupia picha kwenye mtandao wa Instagram inayomuonesha akiwa amejichora ‘tatoo’ kifuani yenye jina la Kajala na kuzua maswali mengi kwa mashabiki wao.
Baada ya kuinyaka picha hiyo huku vyanzo mbalimbali vikieleza wawili hao ni wapenzi, mwanahabari wetu alimtafuta Quick ili aweze kueleza kama wameamua kuweka mambo hadharani kwa staili ya mtandao, alipopatikana, alifunguka:
“Mimi mwilini nimemchora mama yangu kwa sababu nilikuwa nampenda na kumthamini sana na kwa Kajala ni mtu ambaye nakubali kazi zake na kile anachofanya na ni watu ambao pia tunashirikiana kwa kazi mbalimbali za sanaa ndiyo maana nimechora jina lake,” alisema Quick.
Kwa upande wake Kajala, alipoulizwa kuhusiana na kuchorwa jina lake kifuani na kuweka wazi kama wana uhusiano wa kimapenzi na Quick, alisema hapendi kuzungumzia suala hilo.“Mimi nisingependa kuzungumzia chochote kuhusu hiyo ishu maana wajuaji wameshaongea mengi,” alisema Kajala.

Note: Only a member of this blog may post a comment.