Tuesday, October 13, 2015

Anonymous

Shutuma za MAGUFULI Kutumia Bendera ya Taifa na Wimbo wa Taifa Katika Matangazo ya Redio na TV

Jana usiku nilikuwa naangalia habari kwenye kituo kimoja cha runinga. Likatoka tangazo likimuonyesha Dr. Magufuli akijieleza kwa unyenyekevu kwa watazamaji akiomba kura, nyuma kulikuwa na background ya bendera ya Taifa na pia hata vituo kadhaa vya radio nimesikia mara kadhaa wakitoa tangazo la huyo huyo Magufuli na wimbo wa Taifa ukipigwa.
Maoni yangu: 
Kwa kuwa uchaguzi bado basi vyama vya siasa vizuiwe kutumia wimbo na bendera ya Taifa kwenye kampeni zao. Badala yake watumie nembo na bendera zao na ikibidi nyimbo za vyama vyao vinginevyo naona hii haiko vizuri.
By Sajenti/Jamii Forums

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.