Gladness Mallya
MWANADADA staa wa filamu Bongo, Rose Ndauka amesema hataki
kujihusisha na harakati za siasa kwa sasa kwa vile anaogopa
kuwachanganya mashabiki wake.
Akipiga stori na gazeti hili, Rose alisema kwa kuwa yeye ni kioo cha
jamii anayeelimisha kupitia kazi yake, alisema kujiweka wazi upande
ulipo ni kuwagawa watu wake kitu ambacho asingependa kitokee.
“Wasanii wanaozunguka kwenye kampeni hawafanyi vibaya, lakini mimi
siwezi na sikutaka kufanya hivyo ila kura nitapiga na kuhusu ni nani
nitakayemchagua kuwa rais ni siri yangu,” alisema nyota huyo ambaye
anakiri kuwa soko lao limeyumba.
Note: Only a member of this blog may post a comment.