
LOWASSA Ameandika hivi:
"Tutapunguza
misamaha ya kodi kufikia asilimia moja (1%) tu ya pato la taifa (au
chini ya hapo) kama inavyoshauriwa na Shirika la Fedha la Kimataifa
(IMF). Wenzetu Kenya na Uganda wameweza. Tanzania inapoteza zaidi ya
Shilingi trilioni moja nukta nne kila Mwaka kutokana na misamaha holela
ya kodi. - Tukilitekeleza hili pekee, tutaweza kulipa Deni la Walimu la
Shillingi Bilioni Thelathini na Tatu na bado chenji kubwa ikabaki
kuboresha maslahi ya Polisi, Madaktari, n.k. - Kwa mujibu wa Wizara ya
Fedha, kiasi cha misamaha ya kodi katika mwaka wa fedha 2014/15 kilikuwa
Shilingi Trilioni 1.419. Katika kipindi hicho, serikali ilitegemea
kukusanya takriban Shilingi Trilioni 10 kama kodi. Hii inaonyesha kwamba
kiasi cha misamaha kilikuwa asilimia 14 ya mapato ya kodi.
Kuhakikisha kwamba misamaha yote ya kodi inawekwa wazi na inakaguliwa na mamlaka ya kodi (TRA), Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Fedha Za Serikali (CAG), pamoja na Kamati husika za Bunge".
Kuhakikisha kwamba misamaha yote ya kodi inawekwa wazi na inakaguliwa na mamlaka ya kodi (TRA), Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Fedha Za Serikali (CAG), pamoja na Kamati husika za Bunge".
(Share Zaidi Ujumbe Ufike Kwa Wahusika)
Note: Only a member of this blog may post a comment.