Naibu Katibu Mkuu Mpya wa Wizara
ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia Ndugu Emannuel Kalobelo akila kiapo
mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es salaam leo.
Naibu Katibu Mkuu mpya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Ndugu Tixon Nzunda akila kiapo mbele ya Rais Kikwete leo.
Katibu Tawala mpya wa mkoa wa
Katavi Mhandisi Madeni Kipande akila kiapo mbele ya Rais Dkt.Jakaya
Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es salaam leo na kukabidhiwa miongozo ya
kazi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na
katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue(wapili kushoto) wakiwa katika
picha ya pamoja na waliapishwa keo. Kushoto ni Katbu Tawala Mkoa wa
Katavi Ndugu Madeni kipande, wanne kushoto ni Naibu katibu Mkuu mpya wa
Wizara ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia Ndugu Emmanuel Kalobelo na
kulia ni Naibu Katibu Mkuu Mpya Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa
Umma Ndugu Tixon Nzunda.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo amewaapisha manaibu katibu wawili
wa wizara na Katibu Tawala wa mkoa katika hafla fupi iliyofanyika ikulu
jijini Dar es Salaam.
Manaibu katibu walioapishwa ni pamoja Ndugu Emmanuel Kalobelo
anayekuwa Naibu Katibu mkuu Wizara ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia
na ndugu Tixon Nzunda nayekuwa Naibu Katibu Mkuu,Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma.
Katika hafla hiyo Rais Kikwete amemwapisha Mhandisi Madeni kipande kuwa katibu Tawala wa mkoa wa Katavi .
(Picha na Freddy Maro)
Note: Only a member of this blog may post a comment.