
Mgombea
Urais kwa tiketi ya CCM, Dk John Magufuli akiingia kwenye viwanja vya
Himo sambamba na mgombea ubunge wa jimbo hilo, Innocent Shirima
‘aliyenyoosha mkono’.
Magufuli akijinanadi sambamba na mgombea ubunge wa jimbo la Rombo, Samora Kanje.
Magufuli akimwaga sera kwa wakazi wa Jimbo la Vunjo na kuwaahidi vunjo ya neema na amani.
Magufuli akisistiza jambo wakati akizungumza na wakazi wa Mwanga.
Magufuli
akiwaeleza wakazi wa Ndungu Same Mashariki, uchapakazi wa Anne Kilango
na jinsi atakavyoshirikiana nae kiukaribu kwa maendeleo ya jimbo la Same
Mashariki endapo atakuwa rais.
Magufuli akizungumza na wakazi wa Same Mjini
Wakazi wa Hai Jimbo la Vunjo wakifurahia barabarani muda mfupi kabla ya Magufuli kufika jimboni hapo.
Wakazi wa Himo Jimbo la Vunjo wakimsikiliza Magufuli ‘hayupo pichani’.
Wakazi wa Mwanga wakimsubili kumsikiliza Magufuli.
Wakazi wa Tarakea Wilayani Rombo mkoa wa Kilimanjaro wakisikiliza sera za Magufuli.
Maafande wakiwa tayari kwa lolote wakati magufuli akiongea na wakazi wa Rombo mkoani Kilimanjaro.
Wakazi wa Tarakea Wilayani Rombo mkoa wa Kilimanjaro wakisikiliza sera za Magufuli
Wakazi wa Tarakea, Rombo na tabasamu la kumuona Magufuli.

Wakaziwa Ndungu, Same Mashariki wakimsikiliza Magufuli.
Mgombea urais kwa tiketi ya CCM Dk John Pombe Magufuli, jana
aliendelea na mikutano ya kampeni zake za kuwania urais katika Mkoa wa
Kilimanjaro ambapo alifanya mikutano zaidi ya nane.
Magufuli alifanya mikutano katika maeneo ya Tarakea wilayani Rombo,
Himo katika jimbo la Vunjo, Njia panda ya Himo, Mwanga, Kijiji cha
Ndungu kilichopo Same Mashariki na kumalizia na Same Mjini katika
viwanja vya Kwasakwasa ambapo umati mkubwa wa watu ulifurika kusikia
sera za Magufuli.
Akizungumza na wakazi hao Magufuli aliendelea kunadi sera zake za
kutengeneza barabara za lami maeneo hayo, kumaliza migogoro ya ardhi,
kutatua tatizo sugu la maji, kupunguza kodi ya pembejeo za kilimo na
dawa za mifugo.
Magufuli aliwaahidi wananchi hao kuibadilisha Tanzania na kuwa mpya yenye neema huku akifafanua jinsi atakavyoleta mabadiliko.
PICHA NA RICHARD BUKOS/GPL ALIYEKUWA KILIMANJARO
Note: Only a member of this blog may post a comment.