Weekend hii Ligi Kuu soka Tanzania bara inaendelea kwa michezo kadhaa kupigwa katika viwanja tofauti tofauti, miongoni mwa michezo ambayo inatazamiwa kuwa na ushindani mkubwa ni mchezo kati ya Mbeya City dhidi ya Simba, mechi ambayo itapigwa katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Wachezaji wa Simba wakiwa pamoja mazoezini
Naomba nikusogezee picha za mazoezi ya Simba wakiwa jijini Mbeya kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo. Simba wakiwa na kocha wao muingereza Dylan Kerr na msaidizi wake Selemani Matola wameendelea na mazoezi ya kukinoa kikosi chao kuelekea mchezo huo utakaochezwa Jumamosi ya October 17 uwanja wa Sokoine Mbeya.
Hamis Kiiza akifanya mazoezi ya viungo
Kocha wa Simba Dylan Kerr akiongoza mazoezi kwa wachezaji wake
Kocha msaidizi wa Simba Selemani Matola akiwa na mkuu wake Dyalan Kerr wakijadiliana jambo
Note: Only a member of this blog may post a comment.