Wednesday, October 14, 2015

Anonymous

Nyerere Day, Mwapachu na CCM?, Rais JK Bagamoyo, Lowassa Geita + Umeme mgao umeisha? (Audio).


Uchambuzi wa magazeti @CloudsFM umekupita? Ninazo zote zilizoweka headlines kwenye kurasa za magazeti leo 0ctober 14 2015… kama hukupata muda wa kuzisikia zote karibu ucheki na hizi nyingine hapa chini kufidia. 

Leo ni siku ya kumuenzi Baba wa Taifa Mwl Julius K. Nyerere na taifa linaomboleza miaka 16 toka Baba wa Taifa afariki dunia.. lakini maadhimisho wa Mwl. Nyerere  mwaka huu yamekuwa ya tofauti kidogo kwani zimebaki siku 11 tu kufikia Uchaguzi Mkuu wa October 25 2015… hotuba na nasaha zake zinatolewa kila siku kwenye maredio na Television kuelekea uchaguzi huu wa kihistoria na zimeendelea kutoa ujumbe mzito kuenzi amani, umoja na mshikamano wa Taifa… ni tukamuenzi Mwl. Nyerere sio tu kwa hosia wake kwa maendeleo ya Nchi bali kuyaenzi yale aliyokuwa akihubiri kwa vitendo na sio kwa kuzisaliti fikra zake kwa unafiki, uongo na ufisadi uliopitiliza. 

Jana wagombea Urais kupitia CCM na CHADEMA waliendelea na kampeni katika mikoa ya Lindi na Geita kila mmoja akinadi ilani yake kwa wananchi… akiwa Lindi mgombea wa CCM Dk. John Magufuli alisema atahakikisha huduma za afya zinapatikana na kuboresha huduma za Bima za afya ili kila mwananchi apate huduma anayoistahili, pia kuboresha barabara za Kilwa ili kuinua utalii. 

Akiwa Geita, mgombea Urais kupitia CHADEMA Edward Lowassa amesema akiingia madarakani atakachoanza kukifanyia kazi ni kufumua mikataba yote ya madini ambayo haiwasaidii Watanzania na jamii, na atakuwa rafiki wa wachimbaji wa dogo, atatatua tatizo la ajira kwa vijana. 

Balozi Juma Mwapachu atangaza kujitoa CCM kwa kile anachodai ni uvunjifu wa kanuni za katiba ya CCM na kumuenzi Mwl Julius Nyerere angependa kufanya maamuzi magumu na kujitoa na CCM na hatagemei kujiunga na chama chochote kile kuanzia sasa … Mwili wa aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara Abdallah Kigoda kuwasili leo saa nane mchana kutoka India. 

Rais Jakaya Kikwete kesho anatarajia kuweka jiwe la msingi katika Bandari ya Kimataifa ya Bagamoyo kwa ajili ya uzinduzi wa awamu ya kwanza wa ujenzi wa Bandari hiyo… na sasa hivi umeme kukatika itakuwa historia baada ya kukamilika kwa mitambo ya kuzalisha umeme kwa kutumia gesi.
Unaweza kusikiliza uchambuzi wote wa magazeti #PowerBreakfast kwa kubonyeza play hapa chini.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.