Wednesday, October 14, 2015

Anonymous

Je, Wajua?! Hii Hapa Inakuja, Safari Ndefu Zaidi ya Ndege Angani Kwa Saa 19 Bila Kutua

Kampuni kubwa ya Ndege Duniani ya Emirates ilitangaza kuanza safari ya Ndege zake kutoka Dubai mpaka Panama ambayo itaanza mwezi February 2016… hiyo ni safari yenye umbali wa Kilometa 13, 820 na iliingia kwenye hesabu kubwa kwa kuwa safari ndefu zaidi ya Ndege Duniani inayochukua mpaka saa 17 na dakika 35, inakuja Rekodi kubwa zaidi !!
Kampuni ya Ndege ya Singapore Airlines iko tayari kuvunja Rekodi hiyo, wao wamejiandaa kuanzisha safari ya Ndege ya umbali zaidi ya Kilometa 15,300.. itachukua mpaka saa 19 angani kutoka Singapore mpaka New York Marekani.
Singapore wameanza hiyo mipango na wanaamini mpaka mwaka 2018 itakuwa imekamilika na safari zitakuwa zimeanza rasmi, hiyo ikianza itakuwa safari ndefu zaidi ya Ndege angani.. kwa sasa Safari inayoshikilia rekodi ya kuchukua muda mwingi zaidi angani ni ya kutoka Sydney mpaka Dallas Marekani kwa Ndege za Shirika la Qantas Airways.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.