Mwigulu
Nchemba Mjumbe wa Kamati ya Ushindi ya Chama cha Mapinduzi akimnadi
Mbunge mtarajiwa wa Jimbo la Busega Dr.Chegeni mapema hii leo.
Mwigulu
Nchemba Jimbo la Busega kwa Dr.Chegeni akisisitiza Wananchi kwenda
kupiga kura kwa wingi,Hakuna namna CCM itashinda kwa kishindo kama
wananchi hawajitokezi kupiga kura,Kura ni kwaajili ya maamuzi makubwa ya
Taifa lako.
Wananchi wa Sumve wakionesha Umoja waokwenye zoezi la kwenda Kuichagua CCM kwa nafasi zote.
Mwigulu Nchemba akimnadi Mbunge mtarajiwa wa Jimbo la Sumve Nd.Ndasa.
Mwigulu Nchemba akiondoka Jimbo laSumve mara baada ya kuomba kura za Urais,Ubunge na Udiwani kwa Chama cha Mapinduzi.
Mwigulu
Nchemba akiwasisitiza Wananchi wasipuuzie jambola kupiga kura,Pia
ameonya wananchi wanaouza vitambulisho vya Kupigia kura kuwa ni kosa la
kisheria na Kila mmoja anapaswa kutunza kitambulisho chake.
Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza Ndg.Anton Diallo,Mwigulu NChemba na Mh.Charles Kitwanga .
Mbunge
wa Jimbo la Misungwi Ndg.Charles Kitwanga akizungumza na Wananchi wake
kuwa ameshajipanga kuhakikisha Miradi yote aliyoiianzisha anaikamilisha
kwa miaka 5 ijayo.
Mwigulu Nchemba akizungumza na Wananchi wa Jimbo la Solwa hii leo.
Mwigulu Chemba akisalimiana na Mgombea Ubunge Jimbo la Solwa ndg.Salum.
Mwigulu Nchemba akiteta Jambo na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida Bi.Azza Hilaly.
Comrade Mwigulu Nchemba akiagana na Wananchi wa Jimbo la Solwa.
Hisia za Mwananchi kwa Rais mtarajiwa Dr.J.Pombe Magufuli.
Mwigulu
Nchemba akizungumza na Wananchi wa shinyanga hii leo "Nawaasa wananchi
wa shinyanga Mjini,Muacheni Masele aendelee kusimamia malengo
yake,ameshaonesha uwezo wa kusimamia shughuli za maendeleo Jimboni na
serikalini.Hakuna haja ya kubadilisha Mbunge wakati hivi sasa ndio
Vijana wanaotegemewa kusimamia Serikali hii ya CCM inayokuja.Ubunge sio
Fashion kwamba kila siku unaweza kubadilisha"Mwigulu.
CCM "Chama kipo Imara"
Wananchi
wakishangilia moja ya sentensi za Mwigulu Nchemba "Mgombea wa CCM
anauwezo wa Kusimamia jambo na likafanikiwa,ameonesha uwezo huo akiwa
waziri nasasatumpatie asimamie Wizara zote".

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza Ndg.Anton Diallo akimnadi Mbunge mtarajiwa kwa awamu ya pili Shinyanga Mjini Ndg.Steven Masele.
Wananchi wa wakifuatilia Mkutano wa kampeni wa Chama Cha Mapinduzi hii leo Shinyanga Mjini.
Mbunge
mtarajiwa wa Chama cha Mapinduzi Shinyanga Mjini Ndg.Steven Masele
akizungumza na Wananchi wake,Ameahidi kuendelea kusimamia ujenzi wa
Viwanda mbalimbali ndani ya Wilaya ya Shinyanga Mjini ambapo hadi sasa
viwanda vitano vimeshajendwa kati ya 12 vinavyotakiwa Kujengwa kwa
Shinyanga.
Mwigulu Nchemba akiagana na Viongozi na Wananchi wa Shinyanga Mjini mara baaada ya Mkutano wa hadhara.
Picha na Sanga Festo Jr.


Note: Only a member of this blog may post a comment.