Leo team Hekaheka inaendelea na kisa cha kijana
aliyekutwa amefariki akiwa nyumbani kwa mama wa mke wake maeneo ya
Magomeni, Dar es salaam na kusababisha utata mkubwa..baada ya jana ndugu
zake kuzungumza leo inaendelea.
Mjomba kaendelea na kusema wakati wakitafakari alipo ndugu yake akiwa
nyumbani kwa marehemu alimsikia mke wake akizungumza na simu chumbani
huku akiwatahadharisha ndugu zake kuwa ndugu wa marehemu wanakwenda
kuwakagua na polisi.
Baada ya muda akaongea na simu tena akiwa mbele ya shemeji zake na
ghafla akaanza kulia akidai mume wake kanyongwa akiwa nyumbani kwa mama
yake.
Mjomba anasema akaondoka hapo na ndugu zake wengine na kukuta watu
wengi wakimtoa ndugu yao ndani ya shimo akiwa tayari amefariki.
Kilichowashangaza baada ya kumwambia mkwe wa marehemu aende kutoa
taarifa Polisi alikataa na kudai anaumwa na miguu huku mke wa marehemu
akishindwa kufika eneo la tukio.
Msikilize hapa Mjomba wa marehemu akiendelea kusimulia tukio zima…
Note: Only a member of this blog may post a comment.