Chande abdallah na Issa mnally
AIBU! Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa
jina la Zuhura maarufu kama Lolo Princessa ambaye ni mpenzi wa kijana
anayejulikana kama Koko Byanco juzikati alijikuta akipata aibu kubwa
baada ya kufumaniwa akiwa na mwanaume mwingine kiasi cha kusababisha
mchepuko huo kujitosa baharini katika ufukwe wa Coco jijini Dar es
Salaam kukwepa kipigo.
Mapema, dawati la Oparesheni Fichua
Maovu (OFM) lilipata taarifa kutoka kwa Koko, akilalamika kuwa amenasa
meseji kwenye simu ya mtu wake, ikionyesha mawasiliano na mwanaume
mwingine, wakipeana ahadi ya kukutana ufukweni siku hiyo, ambazo
zilikuwa na viashiria vyote vya kimahaba.
“Mpaka nimeamua kuja kwenu nataka
mnisaidie jamani maisha yangu hayana amani kabisa, naomba mnisaidie
nimnase mbaya wangu na hii tabia ikome kwa wote wenye mambo kama hayo.
Mbaya zaidi kwao hawajui kama ananisumbua, hivi nataka mashemeji zangu
wamuone ndugu yao anachonifanyia,” alisema Koko.
Baada ya kuwaona huku makamanda wa OFM
wakianza kukusanya ushahidi kwa kupiga picha, mwanaume alishindwa
kuvumilia na kuanzisha timbwili kali kwa mgoni wake, ambaye alipoona
‘jeshi’ kubwa likimsogelea, alilazimika kukimbilia ndani ya bahari huku
akifukuzwa na mwenye mali.

Note: Only a member of this blog may post a comment.