Sunday, August 2, 2015

Anonymous

KURA ZA MAONI CCM! TATHMINI HII HAPA MDAU!

Kura za maoni ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), zimefanyika kwa utulivu katika maeneo mengi nchini, huku baadhi ya maeneo kukiibuka hitilafu zilizosababisha baadhi ya wanachama kulala mahabusu.

Mbali na kura hizo za ndani ya CCM zilizopigwa jana nchi nzima, ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kutokuwepo kwa mmoja wa wagombea wa ubunge katika jimbo jipya la Kibamba, kumesababisha chama hicho kuahirisha uchaguzi.

Mkoani Arusha Katibu wa CCM Kata ya Mjini Kati jijini Arusha, Ally Meku na Katibu wa tawi wa CCM katika kata hiyo, Yakub Shamban wametiwa mbaroni na Polisi, baada ya kukutwa na karatasi za kupigia kura za ubunge na udiwani nyumbani wakipiga tiki.

Meku na mwenzake walitiwa mabaroni majira ya saa sita mchana wakati kazi ya kupiga kura ikiendelea katika ukumbi wa CCM Mkoa, kutokana na ofisi ya kata hiyo kuungua kwa moto siku chache zilizopita.

Akithibitisha kukamatwa kwa makada hao, Katibu wa CCM Wilaya ya Arusha, Feruz Banno alikiri kukamatwa kwa wanachama hao na kuongeza kuwa alikwenda Kituo Kikuu cha Polisi kupata taarifa lakini ilishindikana kuwawekea dhamana.
“Ni kweli wametiwa mbaroni na Polisi tangu saa sita mchana… nimefika Kituo cha Polisi na nitafuatilia dhamana zao baada ya uchaguzi ndani ya chama kumalizika,”  Banno. 

Alipoulizwa kwa nini katibu huyo alipeleka karatasi nusu kituoni na nyingine kubakiza nyumbani kwake, alisema amefanya kosa kwa kukiuka taratibu za uchaguzi na maelekezo aliyopewa kwa kuwa walikubaliana kila kitu kifanyike hadharani.

Akizungumzia tukio hilo kwa njia ya simu yake ya kiganjani, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, alisema hana taarifa rasmi kwa kuwa yupo nje ya ofisi.
Mkoani Mbeya hali ilikuwa shwari isipokuwa kasoro chache zilizojitokeza kwenye baadhi ya maeneo.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.