Thursday, October 8, 2015

Anonymous

Mramba wa TANESCO Hueleweki, Kazi Imekushinda...JIUZURU!


TANESCO iliwaaminisha wananchi kwamba ifikapo July 2015, kabla ya kampeni za uchaguzi kuanza, gesi itakuwa imefika kwenye mitambo iliyoko Kinyerezi na mitambo hii yote itakuwa imewashwa na kufanya mgawo wa umeme Tanzania kuwa historia na kwamba hatutategemea tena umeme wa maji na wa mitambo ya kukodi iliyopo Ubungo; na kwamba bei ya umeme itapungua kwa kiasi kikubwa. TANESCO iliwaaminisha watanzania kuwa mitambo hii ya Kinyerezi inamilikiwa na TANESCO (kwa niaba ya serikali) kwa asilimia 100. Harakati za kufanikisha azima hii ilianza kabla na kuendelea wakati wa mkutano wa bunge la bajeti. Zilifanyika usiku na mchana na zilisimamiwa na waziri wa nishati mwenyewe na zilitangazwa kwenye vyombo vya habari pamoja na TV.

Ilipofika hiyo July mgawo ukaongezeka. Baadaye TANESCO wakatoa maelezo kwamba mitambo inawashwa moja baada ya nyingine na kwamba ifikapo tarehe 14 Septemba mitambo yote itakuwa imewashwa, baada ya hapo mgawo utakuwa historia. Badala yake ilipofika hiyo tarehe hadi sasa mgawo ukawa mkali sana kwa kiwango ambacho hakijawahi kutokea katika historia ya nchi yetu! Juzi wakatueleza kwamba hali hii itaendelea hadi hapo mabwawa ya kuzalisha umeme yatakapojaa. Na kwamba Tanzania itaendelea kutegemea umeme wa maji na siyo wa gesi kama tulivyokuwa tumeaminishwa hapo awali. Na kwamba umeme wa Kinyerezi unaendeshwa na makampuni kadhaa binafsi ya nje;
Kinyume na tulivoaminishwa hapo awali kwamba mitambo hiyo inamilikiwa na TANESCO kwa asilimia 100 (sasa hayo makampuni ya nje yanafanya kazi gani ambayo wahandisi wetu hawawezi kukifanya wala kufundishwa kukifanya?). Na kwamba hadi sasa mitambo ya Kinyerezi inatoa megawati 90 tu - ikiwa na maana (nadhani) umeme tunaopata sasa ni wa mitambo ya kukodi ya IPTL na wenzake kwa gharama kubwa! Mvua za EL nino zinategemewa kuanza hivi karibuni (kwa taarifa za mamlaka ya maji) lakini kwa mwenendo huu tunategemea excuse nyingine kutoka kwa hawa watu na mgawo utakuwa endelevu! Something is fishy somewhere.

Mwanasayansi hapaswi kuwa na kauli za kubadilika badilika, vinginevyo hafai na anapaswa kuachia ngazi. Ilipaswa ifahamike kwa uhakika (kisayansi) mapem kama mitambo hiyo ya gesi itaweza kutuondolea tatizo letu la kutegemea umeme wa maji kabla ya uwekezaji wa mradi huo. La sivyo tungewekeza kwenye umeme utokanao na maporomoko ya maji ambayo yako mengi tu nchini.

Kwa uzembe huu na kauli za kubadilika badilika, CEO Mramba wananchi hawakuelewi, hawatakuelewa na ni vizuri tu ukajiuzuru kwa kushidwa ku perform, la sivyo uwajibishwe. Waachie wengine wenye uwezo wajaribu.
By Dr Akili.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.